Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amempa Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim kufuatia kitendo cha kutunukiwa Nishani ya Juu ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China nishani ambayo inamfanya Dkt. Salim kuwa mwafrika wa kwanza kupewa heshima na tuzo hiyo ya juu katika historia ya China.

Prof. Palamagamba John Kabudi amesema Nishani aliyopewa Dkt. Salim Ahmed Salim anastahili na kuwataka Watanzania wanapopewa majukumu ya Kitaifa kuyafanya kwa uaminifu na uzalendo usiotiliwa mashaka kwakuwa mbali na kumpa muhusika sifa inaleta heshima kwa Taifa zima kama ilivyo kwa Dkt. Salim Ahmed Salim.