Joseph Leonard Haule, maarufu Professor Jay, Mbunge wa jimbo la Mikumi ametoa maoni kuhusu agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa watumishi wa Mungu wahubiri na kutoa mawaidha hadi kwenye kumbi za starehe.

”Tunaweza kubeza kuwa haiwezekani halafu baadaye akafanikiwa, dunia imebadilika unahitaji kupata neno la Mungu mahali popote ila kwenye klabu itakuwa shuguli nzito sidhani kama linawezekana”. amesema Prof Jay.

Ameyasema hayo alipofanya mahojiano na EATV nakuongeza  “mimi sioni kama itaenda kufanikiwa kwa sababu bahati nzuri au mbaya Mkuu wetu wa Mkoa amekuwa anaongea vitu vingi sana ambavyo havitekelezeki sasa nataka nione kwa hili amaejipangaje”.

Aidha Prof Jay ametoa wimbo mpya alioshirikiana na ndugu zake wawili Black Rhyno, Donkoli, Mr Teacher na Simple X uitwao kaza.

Katika hatua nyingine mkali huyo wa hip hop amemtunuku msanii wa kizazi kipya Maua sama, kuwa ndiye malkia wa bongo fleva kutokana na kujituma na kutoa kazi nzuri ameongeza kuwa anastahili kuungwa mkono na wakongwe wa muziki  kama yeye waliopitia vitu vingi mpaka kufanya vizuri katika tasnia hiyo.

Profesa Jay amesema kuwa nyimbo za hip hop zimekuwa hazitoki kupata tuzo kwa sababu  watu hawajiongezi, ndio maana  muziki wa Hip hop umeshindwa kupata tuzo za nje kama muziki wa kuimba  ambapo amesema kuwa moja ya nyimbo zinazaopendwa na kufanya vzuri kwenye jukwaa ni hip hop kwani huimba vitu vyenye uhalisia tofauti naaina nyingine ya muziki.