WASWAHILI wanakuambia malipo ni hapahapa duniani. Baada ya Esma kutamba sana na mpenzi wake mpya, upande wa pili nao umejibu! Aliyekuwa mume wa mrembo huyo Petit Man naye ameibuka na mrembo ‘mkaree’, ‘full’ kumnyoosha!

Huko Instagram mambo ni moto ambapo kipande cha video kimeachiwa kikimuonesha Petit na mrembo huyo wakinyweshana juisi huku wakipigana mabusu ya kufa mtu.

“Oyooo malipo ni hapahapa duniani, Esma aliona yeye tu ndio wa kututambia sasa angalia mwenzake alivyoibuka na mtoto mkaree balaa,” aliandika shabiki aliyejiita Kinde Instagram.Maoni mengi yaliyowekwa kwenye video hiyo yalionekana kumpongeza Petit kwa kunasa mrembo mzuri!