Papa Francis amewashutumu wakosoaji wake kwa kumfanyia hila , na akasema kuwa ”haogopi” mgawanyiko katika kanisa katoliki. Akizungumza baada ya ziara yake baraniu Afrika, Papa amezungumzia suala la makasisi wenye itikadi kali za kikatoliki ambao wamekuwa wakimkosoa, Pope took issue with conservative clergymen who have criticised him.



Wanaoume hao “hawalitakii mema kanisa “, bali kile wanachokijali ni ” kubadilisha mapapa, kubadilisha mitindo, kubuni matawi ya kanisa “, alisema.

Viongozi wa kanisa katoliki wa Marekani waliwahi kukosoa Papa kwa maoni yake.

Hii ni mara ya kwanza kwa Papa kuzungumzia wazi kuhusu uwezekano wa mpasuko ndani ya kanisa katoliki , ambalo lina zaidi ya wafuasi zaidi ya bilioni moja duniani.

Papa Francis alizitoa kauli zake alipokuwa ndani ya ndege iliyomrejesha Roma baada ya ziara aliyoifanya katika mataifa ya Madagascar, Mauritius na Msumbiji.

Alikuwa ameulizwa swali na mwandishi kuhusu mashambulio dhidi yake kutoka kwa viongozi mahafidhina wa kanisa Katoliki , kupitia vituo vya televisheni na tovuti za Marekani.