Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (katikati) akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT). Kikao hicho kimejadili uratibu wa masuala ya Muungano ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa taarifa kutoka katika kila Wizara na kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano katika Jengo la Bima ya Afya Jijini Dodoma. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Muungano Bw. Sifuni Msangi na Bi. Lupi Mwaikambo Mkurugeni Msaidizi Idara ya Muungano.
Bi. Mariam Silim Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Bw. Ezekiel Chundu Mchumi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) wakifuatilia maelezo ya Naibu Katibu Mkuu (hayupo pichani) katika Kikao cha Wakurugenzi wa Sera na Mipango, Tanzania Bara. Kikao hicho kimefanyika hii leo Jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika hii leo Jijini Dodoma.