Baadhi ya mashabiki nchini Sierra Leone wamevamia nyumba ya Nahondha wa Timu ya Taifa hilo,  Umaru Bangura kukosa Penati dakika 90+4 wakati wa mechi muhimu ya kufuzu kwa kombe la dunia ambapo mechi iliisha Sierra Leon akishinda 1-0 dhidi ya Liberia (Agg 2-3)

Mashabiki walitoa hasira zao kwa kuvamia nyumba yake iliyo mji wa Freetown, ambapo waliitupia mawe kuvunja vioo na madirisha

Kama Bangura angefunga Sierra Leon ingesonga mbele.

"Ilikuwa moja ya siku mbaya sana maishani mwangu, siwezi hata kwenda nje kwa sababu sikutarajia aina hii ya uadui kwangu" aliiambia BBC wakati akiwa chumbani kwake