Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini DSM imebaini moja ya Nyumba zake iliyopo eneo la Oysterbay Mtaa wa mawenzi kitalu namba 823 jijini Dsm imeuzwa Kinyemela tangu mwaka 2000 huku Mpangaji aliyepangisha nyumba hiyo akiendesha biashara ya Ufugaji Mbwa na Paka zaidi ya 300.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Lusubiso Mwakabibi pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama na Maafisa wengine walipotaka kuingia katika eneo hilo walipata vikwazo kutoka kwa Dada aliyedai kuwa msimamizi wa eneo hilo ambapo alidai lazima wawe na Appointment maalum na kuwataka kwenda kusubiri nje ya geti licha ya maafisa hao kujitambulisha

Hata hivyo Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Temekei aliamuru kuingia Kwa nguvu na kufanya Ukaguzi na kujionea mamia ya Mbwa na Paka wanaofugwa katika eneo la nyumba hiyo na kushangwazwa na hali waliyoikuta