Rapa wa muziki wa Hip Hop nchini, Nikki Mbishi amevunja ukimya kwa kumpa pongezi msanii mwenzake upande wa Bongo Fleva, Harmonize kwa kuamini anaweza kusimama na kuanzisha familia nyingine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nikki azungumzia kufuatia hatua hiyo aliyopiga mkali huyo kwa kuamua kuanzisha familia yake ya Konde Gang.

Aidha, Nikki ameandika kuwa ilibidi wakina Sugu na ProfessorJay wawe Ma CEO wa kampuni kubwa za muziki lakini hawajaweza kufanya hivyo.