Rapper wa kike kutokea Marekani, Onika Tanya Maraj maarufu kama Nick Minaj  jana Septemba 5, 2019,  ameutangazia umma kustaafu kazi ya muziki.

Staa huyo ametangaza hayo kupitia mtandao  wa Twitter kwamba:

’Nimeamua kustaafu niwe na familia yangu najua kwa sasa mtakuwa na furaha, kwa mashabiki zangu endeleeni kushirikiana na mimi mpaka kifo changu’– Nick Minaj.

Baada ya  kuandika ujumbe huo mashabiki wamekuwa na maswali pasipo na majibu juu ya uamuzi huo uliofanywa na staa huyo.

Rekodi ya mwisho ambayo ilimrudisha kwenye ‘headlines’ mnamo June 21, 2019, inaitwa Megatron ambayo kupitia mtandao wa Youtube imetazamwa na zaidi ya watu 64,011,930.