Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nedy Music anayetamba na wimbo wa ‘Kinomanoma’ aliomshirikisha msanii mwenzake Jux amefunguka kuhusu kumvimbia Jux, na kununiana na Ruby.

Amesema ”Mimi na Jux hatuna na chochote kwa sababu hii ni kazi na sisi hatuko hivyo hata ukitutoa nje ya kazi ilikuwa fresh, tulikuwa tunashauriana vitu kama wasanii ili kuweza kutengeneza kitu kizuri na hatimaye tulikitengeneza hicho” amesema Nedy.

Nedy ambaye mwaka 2018 alipata tuzo ya Afrimma, lakini alitupiwa lawama za kumnunia msanii mwenzake Ruby mara baada ya kuchukua tuzo hiyo, amesema kuwa hakuna ugomvi wala kununiana kati yake na Ruby pia alijaribu kumtafuta kwa kila njia ili aonyeshe upendo na kumshukuru ila kama Ruby anasema hakumshukuru atakuwa muongo.

Aidha msanii huyo amesema yeye hana maneno kama watu wanavyosema, anazungumza kawaida na hachaguliwi cha kuzungumza na sio muongeaji sana huwa anaongea kawaida tu.

Queen Latiffa ataka Nicki Minaj aachwe apumzike
Katika hatua nyingine nedy amekanusha yeye kushindwa kusimama mwenyewe katika nyimbo zake na kufanya nyimbo zake nyingi kushirkisha wasanii wengine huku akiwa bado hajatoa wimbo alioimba peke yake.

”Nenda kasikilize nyimbo zangu zote ‘umute’ niliowashilikisha na utasikia nikiimba utaelewa uwezo wa Nedy ukowapi maana hata wimbo wa one and only nimeuandika” amesema Nedy