Maafisa wa uhamiaji wa Ufilipino wamemkamata mwanamke mmoja raia wa Marekani ambaye alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ninoy Aquino akijaribu kumtorosha mtoto mchanga mwenye umri wa siku 6 akiwa amemficha kwenye begi lake.

Naibu msemaji wa idara ya uhamiaji ya Ufilipino, Melvin Mabulac alisema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 43 alikuwa apande ndege ya kuelekea New York alipokamatwa baada ya mzigo wake kukaguliwa na mtoto huyo kugunduliwa.

 “Yule mtoto alikuwa amefichwa kwenye begi kubwa,” alisema Naibu msemaji wa idara ya uhamiaji ya Ufilipino.