Katika sehemu ya ziara yake kusini mwa Afrika, Mwana mfalme Harry ametembelea nchini Angola ili kuendeleza jitihada za kuondoa mabomu yaliyo ardhini.

Mwana mfalme huyo ameamua kufuata nyayo za mama yake, Princess Diana ambaye mwaka 1997 alitembelea maeneo hayohayo na kutaka kuondoa mabomu yaliochimbwa ardhini.

Princess Diana alijulikana sana kwa kujitolea kwa wahitaji ingawa mafanikio yake hakuyaweka hadharani.

Kwa mfano Diana alifungua kliniki ya kwanza Uingereza kwa ajili ya waathirika wa virusi vya ukimwi mwaka 1987, na kuweza kufanikiwa kubadili tabia za waathirika

Kuhamasisha uwelewa juu ya mabomu yaliyochimbwa ardhini, ni miongoni mwa kosa kubwa lililosababisha apewe talaka na mume wake Prince Wales mwaka 1996.

Kwa miongo kadhaa mabomu ya ardhini yalikuwa yamaetumika katika migogoro mingi.

Mabomu mengi ambayo hayajalipuka yaliachwa wakati wa vita, kipindi ambacho mauaji ya watu yalifanyika kwa wingi au yalilipuka bila kutarajiwa.