Huku kukiwa na tetesi kuwa mrembo Chioma ni mjamzito, Davido ameanza mipango yakufanikisha ndoa yake na mrembo huyo ambayo huenda ikafanyika mwakani.

Kupitia Kwenye mtandao wa Instagram wa Davido amechapisha picha iliyoambatana na ujumbe uliosomeka First of all introduction ikiwa ni ishara kwamba utambulisho ulishafanyika na sasa inasubiriwa ndoa tu.

Kaka mkubwa wa Davido ambaye naye ametangaza kufunga ndoa mwakani Adewale Adeleka ametuma ujumbe kwenye Instagram yake kuipongeza couple hiyo ambayo imeanza kuwa maarufu sana mtandaoni.