Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma ya maji safi na salama na kutoa zawadi kwa wafanyakazi waliofanya vizuri.

Hayo aliyasema wakati wa kikao kazi mkoa wa Ubungo kilichoandaliwa na Ofisi ya kihuduma Dawasa Mkoa wa Ubungo .

Akizungumzia utoaji wa huduma ya maji, Amesema kwa upande wa Wilaya ya Ubungo malalamiko ya maji yamepungua kwa asilimia kubwa tofauti na hapo awali.

“Napongeza uongozi wa DAWASA Ubungo kwa kuweza kusimamia mchakato mzima wa kutoa huduma ya maji hata wakati naenda kuzindua baadhi ya miradi ya maji kwenye Wilaya hii wananchi walikua na shamra shamra kubwa baada ya kukaa muda mrefu bila maji”

Amesema Makori , “katika Wilaya iliyokuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ni hii ya Ubungo na kipindi nateuliwa kuja kuwa Mkuu wa Wilaya nilikuwa napokea malalamiko ya maji kila siku, ila kwa sasa idara ambayo inafanya kazi vizuri ni hii ya DAWASA nawapongeza sana,”


Naye Meneja wa Dawasa Mkoa wa Ubungo, Pascal Fumbuka amesema eneo la huduma linalohudumiwa na Dawasa Ubungo linapokea Maji kutoka mtambo wetu wa Ruvu juu kilasiku lina sifa ya milima na mabonde kijiografia na kupelekea kuwa na mgawanyo wa huduma kulingana na maeneo kwenye kata 10 za Wilaya hiyo.

Amesema,  Dawasa Mkoa kazi wa Ubungo wamedhamiria katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma unafikia asilimia 95 ifikapo 2020, Pia Kuhakikisha Upatikanaji wa huduma ya Maji ni wa uhakika kwa kupunguza migao mikali na kuongeza usukumaji maji milimani.

Aidha, Fumbuka ameeleza mpango mkakati ni Kuhakikisha kuongeza kaya zinazopata maji kutoka 74,837 hadi kufikia 121,187(Sawa na asilimia 100% ya usambazaji wa huduma) pamoja na Kuhamasisha Wananchi kuendelea kupata huduma ya maji kwa njia ya mkopo

Fumbuka ameeleza zaidi, Dawasa wameweka malengo ya Kuhakikisha wanapunguza malalamiko ya wateja wetu na wananchi kwa ujumla kutoka malalamiko 972 (2018/19) hadi malalamiko 0 (sifuri) kwa mwaka huu wa fedha 2019/20 na Kwa kushirikiana na jamii kuhakikisha kiwango cha maji yanayopotea kinapungua kutoka asilimia 25 (2018/19) hadi asilimia 10( 2019/2020) na baadae.

Mkuu wa Wilaya alitoa zawadi kwa wafanyakazi waliofanya vizuri na kuwataka waendelee kuwahudumia wananchi kwa ufanisi mkubwa.

Meneja wa Dawasa Mkoa wa Ubungo, Pascal Fumbuka akielezea mpango mkakati wa Mkoa wa Kihuduma Ubungo wa kuhakikisha wanaongeza  kaya zinazopata maji kutoka 74,837 hadi kufikia 121,187(Sawa na asilimia 100% ya usambazaji wa huduma) pamoja na Kuhamasisha Wananchi kuendelea kupata huduma ya maji kwa njia ya mkopo.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori akiupongeza  uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) kwa kazis nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma ya maji safi na salama na kutoa zawadi kwa wafanyakazi waliofanya vizuri wakati wa kikao kazi cha mkoa wa Ubungo kilichoandaliwa na Ofisi ya kihuduma Dawasa Mkoa wa Ubungo .
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori akitoa zawadi ya vyeti kwa wafanyakazi waliofanya vizuri katika utoaji huduma kutoka vitengo tofauti wakati wa kikao kazi cha mkoa wa Ubungo kilichoandaliwa na Ofisi ya kihuduma Dawasa Mkoa wa Ubungo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori  akitoa zawadi ya vyeti kwa wafanyakazi waliofanya vizuri katika utoaji huduma kutoka vitengo tofauti wakati wa kikao kazi cha mkoa wa Ubungo kilichoandaliwa na Ofisi ya kihuduma Dawasa Mkoa wa Ubungo.  
Wafanyakazi wa DAWASA wakifuatilia kikao kazi cha mkoa wa Ubungo kilichoandaliwa na Ofisi ya kihuduma Dawasa Mkoa wa Ubungo.