Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro dakta Mathayo D.Mathayo ametenga Zaidi ya shilingi million mia moja kwa ajili ya kuibua vipaji na kuimarisha michezo katika jimbo hilo.

Mbunge huyo ambae ameanza kugawa mipira katika kila kata kwa ajili ya maandalizi ya mashinda hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwezi ujao yatashindanisha timu za wanawake kwa upande wa mpira wa pete na wanaume kwa upande wa mpira wa miguu.

Akizungumza na wananchi wa kata zote 20 anazotembelea Mathayo amesema katika kila kata watashindana vijiji kwa vijiji kwa mtindo wa marudiano mara tatu tatu ili aweze kupatikana mshindi kwa upande wa wanawake na wanaume.

“Nataka mshindane kila kijiji na kijiji na kijiji kitakachoshinda kwenye kila kata,kitapata zawadi ya shilingi milioni mbili kwa timu ya wanawake na shilingi milioni mbili kwa timu ya wanaume”alisema Mathayo

Mathayo amesema ametenga shilingi milioni themanini taslim kwa ajili ya timu zitakazoibuka  kidedea katika kila kata.

“Ndugu zangu michezo ni afya michezo ni ajira leo namkabidhi mhe diwani hii mpira lakini asiigawe mpaka nitakapoleta jezi ili muanze mashindano hayo mkiwa na jezi zinazotofautina au mnataka kucheza kienyeji”alihoji Mathayo

Mathayo pia amekuwa akigawa mipira katika shule za msingi na sekondari katika kata mbalimbali jimboni kwake.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi akitoa somo kwa wananchi wa kata ya Same Mjini,Kisiwani na Stesheni kwa njia ya mabango kuhusu kazi kubwa zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dakta Mathayo David Mathayo akiwakabidhi Mwenyekiti wa mji mdogo wa Same Eliamini Mkongo na diwani wa viti Maalum CCM Halima Mgonja fedha Taslim kwa ajili ya maendeleo mbalimbali katika kata hiyo kama alivyoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa Jimbo hilo kwa awamu ya tatu.