Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis (82) jana alichelewa misa katika Kanisa la Mt. Petro, jijini Vatican baada ya kukwama kwenye lifti kwa dakika 25 kufuatia umeme kukatika, kabla ya kutolewa na kikosi cha zimamoto. Awali ilihofiwa kuwa kiongozi huyo alichelewa kutokana na sababu za kiafya.