Mwanamuziki Ray C ameweka picha ikimuonesha akiwa amevaa nguo zinazomuonesha yuko hospitalini, na akiandika kuwaomba watu kumpa ushauri upi wa kufanya ili kuhakikisha mimba haitoki tena.


Kupitia ukurasa waje wa Instagram ameambatanisha "Hashtag" zinazoeleza wazi mimba kuna mimba ambayo alikuwa nayo na tayari imeharibika.

"Naombeni ushauri kina mama wote nifanyaje mimba isitoke? imeniuma imenibidi nishee nanyi My baby is no more, mwanangu kaenda zake,” ameandika  Ray C

Kwenye komenti watu wengi walionekana wakimpa pole na wengine wakimpa ushauri kipi afanye ili hali kama hiyo isitokee tena.

"Ukishika mimba tu tumia Duphaton na Folic Acid kwa miezi 3, mpaka 4 mimba haitotoka pole sana." aliandika mdau mmoja katika komenti.

2018 aliwahi kuweka picha akiwa na mwanaume ambaye kwa mionekano ambayo walikuwa wamekaa ilikuwa inaonesha kuwa ni wapenzi japo hakuandika jambo lolote zaidi ya kuweka tu picha.