MAN United inauwezekano wa kukosa wachezaji sana katika mchezo wao wa leo dhidi ya Leicester City hiyo ni baada ya kuelezwa kuwa Paul Pogba na Anthony Martial wataukosa mchezo huo.Kipute hicho cha Premier League kitapigwa kwenye Uwanja wa Old Traff ord ambapo Pogba ana majeraha ya kifundo cha mguu na ndiyo maana alikosa hata michezo ya timu yake ya taifa ya Ufaransa wiki iliyopita.Wachezaji wengine wa United ambao wapo hatarini kuukosa mchezo huo ni Luke Shaw (nyama za paja), Diogo Dalot (nyonga), Jesse Lingard (mgonjwa) na Aaron Wan-Bissaka (mgongo) huku Eric Bailly akiwa nje muda mrefu kwa jeraha la goti.Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer yupo katika presha kubwa kwa kuwa timu yake imepata ushindi mmoja tu katika mechi nne za ligi hiyo msimu huu.