Waziri wa Nchi ,ofisi ya Waziri Mkuu ,Uwekezaji ,Angela Kairuki akizungumza wakati wa mchezo wa fainali ya Mashindano ya Angela Kairuki Cup 2019 alipoalikwa kama mgeni rasmi ambapo pamoja na mambo mengine alikabidhi zawadi kwa mabingwa wapya wa mashindano hayo.
Katibu wa Cha soka wilaya ya Same,Nathaniel Msuya akisoma taarifa fupi ya mashindano ya Angela Kairuki Cup wakati wa kuhitimisha ligi hiyi iliyodumu kwa muda wa miezi miwili ikishirikisha jumla ya timu 54 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Same. 
Mgeni rasmi katika mashindano hayo ,Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji Angela Kairuki akisalimiana na waamuzi wa mchezo huo.
Waziri Kairuki akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka ya Ujamaa fc Kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali. 
Waziri Kairuki akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kisiwani United kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali baina ya timu hizo mbili.
Mgeni rasmi katika mashindano hayo ,Waziri Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kisiwani united kabla ya kuanza kwa mchezo huo. 
Mgeni rasmi ,Waziri Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na kikosi cha Ujamaa fc kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali kwa timu hizo ,kulia ni mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Isaya Mungulu. 
Baadhi ya Mashabiki wakifuatilia mchezo huo.
Na hivi ndivyo ilivyokuwa wakati mchezo wa fainali baina ya timu za Kisiwani united na Ujamaa fc zikimenyana kuwania ubingwa wa mashindano ya Angela KAiruki Cup 2019 .
Mashabiki wa timu ya Kisiwani United wakishangilia baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa na kutangazwa mabingwa wapya baada ya kuchapa timu ya Ujamaa fc bao 2 kwa 1 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa shule ya Msingi Hedaru.
Sehemu ya zawadi zilizotolewa kwa Mshindi wa kwanza na wa pili katika Mashindano hayo .
 Mgeni rasmi ,Waziri Kairuki akikabidhi Kombe kwa nahodha wa timu ya Kisiwani united mara baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya soka ya Ujamaa fc bao 2 kwa 1.
 Waziri Kairuki akikabidhi fedha taslimu ,kiasi cha Sh Milioni 1.5 kwa nahodha wa timu ya Kisiwani United mara baada ya kuibuka Mabingwa wapya wa mashindano hayo.
Waziri Kairuki aikabidhi pipikipi kwa Nahodha wa timu ya soka ya Kisiwani United baada ya kuibuka mapbingwa wapya wa mashindano hayo. 

Na Dixon Busagaga ,Moshi.
 
Mabingwa wapya wa mshindano ya Angela Kairuki Cup 2019 timu ya Kisiwani united  wamekabidhiwa zawadi zao ambapo wamefanikiwa kijinyakulia zawadi ya Ng'ombe pesa taslimu kiasi cha sh Mil 1.5,Pikipiki moja, na Medali 25 kwa Wachezaji.


Zawadi kwa mabingwa hao wapya zimekabidhi na Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji, Angela Kairuki mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali kati ya timu ya Kisiwani United   kutoka kata ya Kisiwani dhidi ya  timu ya Ujamaa fc, ambapo Kisiwani walifanikiwa kushinda kwa mabao mawili kwa moja.

Mshindi wa pili katika mashindano hayo,timu ya Ujamaa fc wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni moja, Medali na pikipiki huku mshindi wa tatu,timu ya Kiwanja fc akiambulia kiasi Cha sh laki tano pamoja na medali.


Katika mchezo huo mabao ya washindi yalipachikwa na Wachezaji Ally Rajab kunako dakika 35 ya kipindi cha kwanza huku mchezaji Juma Makumbi  akipigilia msumari wa pili uliowapatia ubingwa timu ya kisiwani fc.


Bao kwa upande wa timu ya soka ya Ujamaa fc iliyokuwa imesheheni wakongwe limefungwa na mchezaji Ezekiel Ombeni kunako dakika ya 40.

Katika mchezo huo ilishuhudiwa mchezaji Ally Mbaga akitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa mwamuzi wa pembeni wakati akilalamikia maamuzi yake dhidi ya bao lililofungwa n timu ya Ujamaa fc.

 
Mashindano ya Angela Kairuki Cup yamekuwa yakifanyika kila mwaka katika wilaya ya Same na kushirikisha timu kutoka kata 32 za wilaya hiyo huku mdhamini Mkuu wa mashindano hayo ,Wazxiri wan chi,ofisi ya Waziri Mkuu ,uwekezaji ,Angela Kairuki akiahidi kuendelea kuyadhamini kwa miaka mitano.