Mwanamke mwenye umri wa miaka 73 katika jimbo la Kusini mwa Idia la Andhra Pradesh amejifungua watoto 2 mapacha wa kike.
Wazazi waliomsaidia kujifungua mapacha hao wanasema amejifungua kwa njia ya kuanguliwa kwa mayai yake ya uzazi nje ya mfuko wa uzazi na baadae kuchanganywa na mbegu za kiume na kisha kupandikizwa ndani ya mfuko wake wa uzazi ama IVF kwa lugha ya kitaalamu. Alipatiwa kwanza matibabu ya IVF, Siku ya Alhamisi.

"Mama na watoto kwa pamoja wanaendelea vizuri,"Dkt. Uma Sankar ameimbia BBC.

Mangayamma Yaramati amesema yeye na mumewe ambaye ana umri wa miaka 82, wamekuwa wakati wote wakutaka kuwa na watoto lakini hawakuwahi kupata mtoto hadi sasa.

"Tumefurahi sana ,"mesema mume wake, Sitarama Rajarao, akiongeza kuwa mkewe alipata ujauzito katika kipindi cha miezi miwili tu baada ya kufanyiwa matibabu ya IVF.

"Tulijaribu mara nyingi kupata watoto na tukawatembelea madaktari wengi ," Amesema Bi Yaramati , "kwa hiyo hiki ni kipindi cha furaha zaidi maishani mwangu ."

Aliongeza kuwa alihisi kutengwa na jamii na wanakijiji wenzake na mara kwa mara amekuwa akitengwa katika mikusanyiko kwasababu yeye hakuwa mama.

Anasema :"walikuwa wananiita mwanamke asiye na mtoto ,"

Lakini siku ambayo watoto wake mapacha walipozaliwa, Bwana Rajarao alipata kiharusi. Kwa sasa anapokea matibabu hospitalini.

Mapacha hao wasichana walizaliwa kwa njia ya upasuaji , jambo ambalo ni la kawaida kwa uzazi huo wa nadra.

Mnamo mwaka 2016, mwanamke mwingine wa India aliyekuwa na miaka 70 , Daljinder Kaur, alijifungua mtoto wa kike.
Chanzo - BBC