Staa wa kike wa muziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka kuhusu tuhuma za kuwahonga pesa wanaume ambao anakuwa nao katika mahusiano.


Lulu Diva ameiambia EATV & EA Radio Digital wakati akijibu tetesi hizo kuwa yeye hawezi kumpa pesa mwanaume kwa sababu mwanaume ndiye anatakiwa kuhangaike kwa ajili yake, isipokuwa pesa yake anaweza kumpa mama yake au ndugu yake pekee.

“Hamna mtu ambaye naweza kumpa pesa yangu zaidi ya ndugu yangu, mzazi wangu na familia yangu labda niwe nimependa au kwa mtu mwenye uhitaji lakini sio kutoa pesa yangu mfukoni kumpa mwanaume haiwezekani, yeye atakuwa anafanya kazi gani asinihonge mimi”, amesema Diva.

Lulu Diva ameendelea kusema kuwa kufanya kitu hicho hawezi hata kama hakupende, kwa sababu bado anatafuta na hana muda wa kumsaidia mtu pesa, labda kila mtu ajikimu kivyake wakiwa kwenye mahusiano ila sio kutoa pesa.