Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Masawiliano wa Benki ya CRDB, Tully Ester Mwambapa (kushoto) wakati wa matembezi yao kilometa tano (5KM) yaliyoambatana na mbio za nyika za Brazuka (Brazuka Marathon 2019) kwa ajili ya kuchangia watoto wanye matatizo ya moyo, zilizofanyika Septemba 15, 2019 katika viwanya vya JK Pack, jijini Dar es salaam. Mbio hizo zilidhaminiwa na Benki ya CRDB.
Washiriki wa  matembezi ya kilometa tano (5KM) yaliyoongozwa na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete wakiendelea na matembezi ya yao yaliyoambatana na mbio za nyika za Brazuka (Brazuka Marathon 2019) kwa ajili ya kuchangia watoto wanye matatizo ya moyo, zilizofanyika Septemba 15, 2019 katika viwanya vya JK Pack, jijini Dar es salaam. Mbio hizo zilidhaminiwa na Benki ya CRDB.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete amesema waandaji wa mbio za nyika za Brazuka kwa ajili ya kuchangia watoto wanye matatizo ya moyo, wamefanya jambo jema katika kuokoa maisha ya watoto zaidi ya 500.

Dkt Kikwete katika mbio hizo alishiriki kwa kutembea Kilomita Tano (5KM) ikiwa ni kuimarisha afya pamoja na kuunga mkono marathon hizo za kuchangia watoto hao.

Akizungumza baada ya kumalizika mbio hizo, Dkt. Kikwete amesema kuwa licha ya kuchangia watoto hao kwa walioshiriki kwa mwitikio mkubwa wameimarisha afya kwa kutoa sumu mwilini.

Amesema kuwa kwa waandaji Brazuka waendelee kuandaa marathon hizo kwa kila mwaka kutokana na kuwepo kwa mwitikio wa jamii katika uchangiaji fedha zitakazosaidia watoto wenye matatizo ya moyo na kuokoa maisha yao.

Aidha amesema kuwa benki 18 ikiwamo Benki ya CRDB zilizoshiriki katika marathon hizo wamejitoa katika kufanikisha marathon hizo kwa wao wenyewe kukimbia.

Dkt. Jakaya Kikwete amewashukuru wadhamini kwa kutoa mchango yao katika kufanikisha mbio hizo za marathon.

Naye Mratibu wa Marathom hizo za Brazuka, Nasikiwa Berya amesema kuwa ni mara ya kwanza kuandaa mbio za nyika hivyo wataboresha changamoto zilizojitokeza katika marathon hizo.

Amesema kuwa mwitikio wa marathon hizo umekuwa mkubwa na kufanya kumtia moyo wa kuendelea kuzifanya ikiwa ni kupokea maagizo ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ya kufanya kila mwaka.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi amesema kuwa marathon kwa ajili ya watoto wenye matatizo ya moyo ni jambo muhimu ili kuweza kuwatibia katika taasisi hiyo.