Marekani imetangaza mipango ya kutuma vikosi vya kijeshi nchini Saudia kufuatia mashambulizi dhidi ya hifadhi za mafuta za taifa hilo.Marekani kutuma wanajeshi Saudia

Waziri wa ulinzi Mark Esper aliambia wanahabari kwamba wanajeshi hao wataelekea katika taifa hilo ili kuimarisha ulinzi . Hatahaivyo idadi yao bado haijajulikana.

Waasi wa Houthi nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran wamesema kwamba walihusika na mashambulizi ya visima viwili vya mafuta wiki iliopita. Lakini Saudia na Marekani zimelaumu Iran kwa mashambulizi hayo.

Siku ya Ijumaa , rais Trump alitangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran huku akisema kwamba alipendelea kuzuia mgogoro wa kijeshi.

Vikwazo hivyo vipya ambavyo rais Trump alivitaja kuwa vya kiwango cha juu vitalenga benki ya Iran na mali yake iliopo ugenini.

''Nadhani kujizuia ni muhimu'' , aliambia afisi ya White House.

Lakini siku ya Jumamosi. Kamanda wa jeshi la Iran Revolutionary Guard IRGC alisema kwamba taifa hilo litamuangamiza mchokozi yeyote.