Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amekemea tabia ya baadhi ya Makamanda wa Polisi nchini kujihusisha na shughuli za kisiasa kwa kile alichoeleza kuwa ni kinyume na Katiba ya nchi.

Akizungumza kwenye kikao chake na Wakuu wa Jeshi la Polisi wa Mikoa, IGP Simon Sirro amesema hata jeshi hilo linashangazwa na baadhi ya maafisa wake kujihusisha na siasa.

"Baadhi yetu kujiingiza kwenye harakati za kisiasa si sahihi, kwa mujibu kwa Katiba yetu, lakini kwa 'ushahidi' unashindwa kabisa kujua maadili yako unatakiwa kufanya nini kwenye umma"

“Watu wanataka kusikia unasema nini, wewe sio mwanasiasa unajiaibisha mwenyewe, tujikite kwenye majukumu yetu hayo unayofanya umeyatoa wapi.?

“Halafu unafanya hivyo kwa sababu uko kwenye nafasi hiyo tukikutoa hapo utaweza kufanyia nyumbani kwako? Si Pahala pa kufurahisha watu, wengine wanafanya vitu  kutafuta umaarufu wa kisiasa tu, unamfurahisha nani?” Amesema IGP Sirro