Msanii Harmorapa asiyeishiwa na vituko hapa nchini, ametoa kali ya mwaka baada ya kubebwa kwenye machela wakati wa uzinduzi wa filamu 2 za Duma, zilizofanyika Mlimani City na kusema kuwa watanzania wasimbeze kwani anayo mahusiano mazuri na nyota wa HipHop duniani Jay Z.


Akiwa mbele ya waandishi wa habari, Harmorapa akazungumzia muonekano wa mavazi yake katika tukio hilo.

“Mimi ni mnyamwezi siku zote unajua , imenigharimu kiasi kikubwa sana halafu vitu vyangu vinakuwa 'Proffesional' sana na sio 'local' ila nahisi watu hawajawahi kuniona na huu muonekano”amesema Harmorapa. 

Kwa upande wa mahusiano yake na mwanaHipHop maarufu duniani Jay Z, Harmorapa amesema

“Jay Z ni shemeji yangu na nina kolabo kubwa ya dunia ambayo nafanya naye inakuja, kwa sasa tupo katika mchakato wa kufanikisha hilo na itatoka muda si mrefu” amesema Harmorapa.

Kufuatia Kolabo hiyo Harmorapa anataka kuwaonesha watanzania kwamba anachokifanya anakijua na kwamba waache kumchukulia poa kwa kuwa hajakurupuka.