Muigizaji wa Bongo Muvi, Ester Kiama amesema muigizaji mwenzake, Wema Isaac Sepetu amemuumiza roho hadi kumfanya aangue kilio na kukosa raha siku nzima. Ester ameyasema hayo kufuatia hivi karibuni Wema kumjibu mmoja wa mashabiki wake kwenye Mtandao wa Instagram ambaye alimsifia na kumuambia amekosa kitu kimoja tu bila kukitaja ndipo Wema alipomjibu; “ugumba.”


“Kwa kweli ile siku Wema aliniumiza sana. Hakuna siku ambayo nimejisikia vibaya kama siku ile nilivyoona hilo jibu la Wema kuhusu suala la ugumba, niliumia mno na siku yangu ikaharibika, yaani alinifanya siku yangu yoyote isipite bila kumuombea,” alisema Ester.

Kwa muda mrefu Wema amekuwa kwenye changamoto ya kutopata ujauzito, lakini hata hivyo hivi karibuni alikaririwa akisema tatizo hilo limeshatatuliwa na sasa anaweza kupata ujauzito.