Siku moja baada ya msanii Nay wa Mitego ku-post video Instagram akiwaponda wasanii kuwa na mabaunsa wa kuwalinda, msanii wa filamu Duma amepingana na kauli ya Nay wa Mitego baada ya yeye kuonekana na mabaunsa watatu usiku wa uzinduzi wa filamu yake.


"Mabaunsa hawa wananilinda kwa ajili ya tukio hili kubwa na la kihistoria, nikaona sio mbaya nikaingia na watu wakani 'support' kwa namna moja au nyingine ni kitu kizuri lakini huwezi kujua watu wanaweza wakakuvamia kwa sababu hapa watu ni wengi na wengine wanaweza wasiwe wazuri kwa upande wangu".

Kupitia ukurasa wake wa instagram Nay wa Mitego aliandika, ''sasa hivi kutembea na mabaunsa imekuwa 'fashion' sio kama usalama wa mtu, maana naona hata 'video queen', wadangaji, DJ's na wao wana mabaunsa, pia wasanii wengine hawana sababu ya kutembea na baunsa kwanza hawana hela".

Baada ya kipande hicho cha video kukiachia, kilionekana kupendwa na watu wengi na ndani ya muda mfupi kilikuwa na watazamaji 124,426 , kilipendwa (likes) 36,293, pamoja na maoni ya watu 2,235.