Msanii maarufu kutoka nchini Tanzania, Harmonize, kwa sasa ameaga ukapera rasmi baada ya kufunga pinga za maisha katika hafla ya kisiri iliyoandaliwa siku ya Jumamosi, Aprili 7

Jambo la kushangaza ni kuwa hakuna mwanamuziki yeyote wa Wasafi alihudhuria hafla hiyo wala kuweka taarifa hizo kwenye mitandao jamii.

Wanamuziki kama vile Diamond, Rayvanny, Lavalava na nyota wengine wa WCB walisusia harusi hiyo huku kukiwa na ripoti kuwa Harmonize anapania kujitenga na kampuni hiyo.