Basi la Mwendokasi imeungua muda huu Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam. Watu wamefanikiwa kutoka mpaka sasa linaendelea kuungua japo juhudi za kizima moto zinaendelea. Chanzo cha ajali bado hakijafahamika.
Angalizo: Kutokea tukio hilo la Moto foleni ni kubwa, hivyo watumiaji wa barabara ya Morogoro tafuteni njia mbadala zikiwemo za Goba na Makongo Juu au Kinyerezi. Habari kamili zitawajia punde.