Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

BARAZA la Wafamasia limesema kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) hawana budi kwenda na teknolojia hiyo kwa kuweka mfumo kwa wafamsia wote nchini kutumia kujifunza vitu mbalimbali vinavyotokea ikiwemo masuala ya dawa.

Hayo ameyasema Msajili wa Baraza hilo Elizabert Shekalaghe katika maadhimisho ya siku ya wafamasia Duniani kwa baraza kuzindua mfumo taarifa mbalimbali ambazo wafamasia wanatakiwa kufuata yaliyofanyika jana katika ofisi ndogo za baraza hilo jijini Dar es Salaam amesema kuwa mfumo huo utarahisisha wafamasia hao kupata taarifa kwa kila wakati pamoja na leseni zao kwa katika mfumo.

Amesema kuwa katika mfumo kutafanya wafamasia kupata huduma zote katika mtandao na hakuna sababu ya kwenda katika ofisi za baraza.

Shekalaghe amesema kukiwepo na dawa mpya imeingia basi wafamasia wote watapata taarifa katika mtandao pamoja na dawa ambayo si salama kwa binadamu.

“Dunia inakwenda kwa kasi hivyo nasi lazima twende kwa kasi hiyo katika mabadiliko ya utoaji wa huduma katika mfumo wa mtandao na kurahisisha utoaji huduma bora za afya kwa wananchi”amesema Shekalaghe.

Aidha amesema kuwa wafamasia wanatakiwa kufuata sheria,Kanuni pamoja na taratibu na wataokwenda kinyume baraza halitaweza kuvumilia kwani kuachwa kwa mtu kuna haribu taasisi na kufanya wananchi kukosa imani utendaji wa Baraza hilo.

Nae Mwenyekiti wa Baraza hilo Legu Mhangwa amesema kuwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa wafamasia ni muhimu sana katika maendeleo ya afya za wananchi katika utumiaji wa dawa.

Mhangwa amesema baraza limefanya kazi kubwa katika kuunda mfumo huo hivyo lazima utumike na kuleta matokeo chanya kwa wafamasia.
Msajili wa Baraza la Wafamasia, Elizabert Shekalaghe akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wafamasia Duniani iliyofanyika katika ofisi ndogo za Baraza jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafamasia Legu Mhangwa akizungumza kuhusiana na mfumo wa mpya wa mawasiliano uliyoanzishwa na kuzinduliwa katika maadhimisho ya siku ya Wafamasia Duniani.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafamasia Legu Mhangwa akibonyeza kitufe kuashiria kuzinduliwa kwa mfumo wa mawasiliano kwa wafamasia.
Mkuu wa Idara ya Mafunzo wa Baraza la Wafamasia Grace Malange akitoa maelezo kuhusiana na mafunzo yatakayokwepo katika mfumo wa baraza hilo.
Mkuu wa Idara ya Tehama wa Baraza la Wafamasia Yamwaka Gadi akiwapitisha wafamasia katika mfumo katika maadhimisho ya Siku wafamasia Duniani.
Baadhi ya wafamasia walioshiriki katika maadhimisho ya siku ya wafamasia.
Picha ya pamoja ya katika maadhimisho ya siku wa wafamasia.