Mwanamke mmoja nchini Australia amejaribu kuwazuia majirani zake kuchoma nyama kwa kuwashitaki mahakamani.

Cilla Carden kutoka jiji la Perth, Magharibi mwa Australia amedai kuwa shughuli zao za uchomaji nyama, uvutaji wa sigara na kelele za watoto unavunja sheria za makazi ya watu.

Amefuata njia hiyo ya kisheria ili shughuli hizo ziache kufanywa na majirani.

Mahakama ya jimbo imetupilia mbali madai yake kwa kusema kuwa hayana maana na ushahidi wa kutosha.

Madai yalihusisha pia familia zinazoishi jirani yake kupunguza mwanga wa taa zao, kuwanyamazisha wanyama wanofuga pamoja na kuweka miti kwenye bustani zao za kupumzika.

'
Amesema kuwa harufu ya moshi wa sigara na nyama choma zimemsababishia ashindwe kuishi vizuri.

''Siwezi kufurahia sehemu yangu ya kupumzika. Wameweka jiko la nyama choma ili nifikiwe na harufu ya samaki - harufu pekee ninayiopata ni ya samaki tu,'' Cilla Carden ambaye hali nyama ni aliiambia runinga ya Nine news siku ya Jumatatu.

Wanaishi kwenye nyumba yao kama familia
Uongozi wa jimbo hilo ulimjibu kuwa familia hizo zinajaribu kuishi kama familia. Hata hivyo familia waliokua wakilalamikiwa wamehamisha jiko lao la kuchomea nyama kama sehemu ya kumsaidia mlalamikaji.

Mahakama iliongeza pia familia hiyo, wamekua hawawashi taa usiku na kuwazuia watoto kucheza kutokana na hofu walioipata kwa kushatakiwa.

Bi Carden alikata rufaa ya uamuzi huo katika mahakama kuu ya Australia Magharibi, alikabidhi kurasa zaidi ya 400 zenye malalamiko ya kukata rufaa mwezi Machi.

Mwanasheria mkuu wa Mahakama hiyo alisema kuwa kurasa zilikabidhiwa kwa mahakama zinashangaza