Msanii wa Muziki wa Bongofleva, Amber Lulu, amesema moja ya matukio ambayo anayakumbuka akiwa anasoma Shule ya Sekondari Itigi Mkoani Mbeya, alimshushia kichapo, mwalimu wake kwa kile alichokidai alikuwa anamuonewa.


Amber Lulu ametoa kauli hiyo katika kipindi cha Kikaangoni, kinachorushwa kwenye kurasa za Facebook na Youtube ya East Africa TV, kila Jumatano kuanzia saa 8 na nusu mchana.

"Kuna muda mambo yanakufika hapa, kuna Mwalimu tulizipiga kwa sababu alikuwa ananionea sana, alikuwa anatabia moja kila Ijumaa anaitumia meseji eti usipokuja Shule nakuchapa, kumbe yeye alikuwa ananipenda kimapenzi na mimi nilijua alikuwa ananitaka" amesema Amber Lulu

"Kuna siku Jumatatu nimeenda Shule, yeye akaanza kunitoa mbele kuwa sikwenad Jumamosi, na kipindi hicho ilikuwa hatutakiwi kuchapwa matakoni, basi nikampa mkono akanipiga kwenye makalio, nikagoma nikamrudishia na mimi baadaye nikampeleka hadi polisi." amesema Amber Lulu

Katika kipindi hicho Amber  Lulu amesema yeye wakati anamaliza kidato cha nne alipata ufaulu wa Division 2 ya 34 na kupelekea kuzua gumzo kubwa kwenye mitdao ya kijamii.