SIKU chache baada ya video kusambaa mitandaoni ikimuonesha akimwaga machozi huku mashabiki wakienda mbali na kudai atakuwa ameachika, msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka kilichompelekea kuposti video hiyo.   Akipiga stori mbili tatu na Mikito Nusunusu, Gigy alisema anawashangaa ‘wanaomjaji’ kwa kile ambacho hawakijui wakati sababu ya kuposti ni kujiamulia tu na hakuna chochote kilichomtokea.

“Wananzengo jamani hawana dogo, mimi nimeposti tu ile video basi kila mtu kaanza kuongea lake mara ohhh! Nimeachwa na bwana’angu, watasubiri sana na watapata aibu wao kwani hakuna kilichonitokea,” alisema Gigy.