Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe  ameshawasili Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu tayari kwa ajili ya kesi ya 'uchochezi' inayomkabili.

Zitto anatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu mauaji yaliyotokea Nguruka, Kigoma. Kesi hiyo ipo katika hatua ya usikilizwaji ambapo upande wa Jamhuri umefikisha shahidi wake wa tano Dk. Ernest Nsumila ambaye aliyetoa ushahidi wake tarehe 16 Julai 2019

Katika kesi hiyo, Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi ambayo anadaiwa kuyatenda tarehe 28 Oktoba 2018 katika mkutano na waandishi wa habari, uliyofanyika kwenye Makao Mkuu ya Ofisi ya Chama cha ACT Wazalendo.