SERIKALI ya Kenya imemkamata mchungaji mmoja nchini humo aliyemleta Yesu bandia na kuwadanganya waumini wake kuwa Yesu karudi.
Yesu huyo bandia, anayetumia jina la Michael Job, alikuwa akikusanya fedha za waumini akiwaambia kuwa atakaporudi mbinguni angewaandalia makao ya kudumu huko, kwa hiyo alihitaji pesa za kununulia saruji, mabati, nondo na matofali.
Wachungaji wengine wawili waliomwalika mtu huyo nchini humo, mwenye uraia tata wa Marekani,  wamekamatwa.
Mtu huyo ambaye ni mwinjilisti  wa kanisa la “Jesus Loves You Evangelistic Ministries”,  alitokea akiwa amevalia kama Yesu Kristo kwenye mahubiri ya kidini ya Kiserian Mega Interdenominational Crusade nchini Kenya mwishoni mwa juma lililopita.