Asalaam Alykuum wakubwa.

Kumekuwa na kasumba moja kwenye kiwanda cha mziki wa bongo flava, kuwa pale inapotekea msanii akawa na spot light kubwa anaanza kupambanishwa na Diamond haijalishi huyo msanii yupo upande gani.
Diamond amekuwa kama ndo S.I Unit ya mziki wa bongo flava kuwa kila msanii lazima alinganishwe naye na kupambanishwa iwe kwa heri au kwa shari. Nikikumbuka kipindi Alikiba anaf anya comeback kweny sanaa kuliibuka makundi mawili moja likimshabikia huyu jingine yule. Team zilikuwa kubwa sana ikawa Alikiba na Diamond.

Nakumbuka tena kipondi Darassa anaachia mikwaju ya maana kama ngoma yake pendwa ya mziki watu walianza kumfananisha na diamond akaonekana ni bora kuliko diamond mpk yeye akaonekana upepo kuanza kumpitia akajaa bichwa baada ya hapo imebaki historia tu siyo tena yule darasa wa mziki na wale watu hawana mda naye tena washamsahau.

Aslay naye vile vile watu walimvimbisha kichwa na kupewa tambo kuwa yeye ni mkali kuliko Diamond ikapelkea kujiita nguvu ya Umma but kila mtu anajua Aslay siyo yule tena na wale watu awaliomvimbisha kichwa hawana time naye tena ile nguvu ya Umma haipo tena.

Walewale waliojifny wanamshabikia Alikiba, Darassa, Aslay, ndo hawo hawo waliomrubuni Rich Mavoko kuwa WCB inamnyonya na yeye ni mkubwa kuliko Diamond so hawezi kuwa chini yake hii ikampelekea Mavoko ajitoe WCB kwa mbwembwe kubwa lakini sasa hawana time naye anaachia ngoma kila iitwapo leo lakini zote ziiiii.

Sasa hivi upepo umerudi kwa Harmonize wanamjaza kuwa ashakuwa mkubwa so kuendelea kuwa chini ya Diamond ni kuendelea kunyonywa, bora ajitoe aanze kijisimamia yeye kam yeye. Bila kusahau kuwa ndo hawa hawa waliokuwa wanamponda kuwa hajui kuimba anamuiga boss wake na kujifanya kumkuza Rayvanny kuwa ndo mwenye kipaji, lakini kwa sasa wamegeuza kibao wanamuona Harmonize ndo mkali hata mond hamfikii. Kwa sasa ameshakuwa mkubwa basi haina haja ya kuendelea Kuwa chini ya WCB.

Upepo huu naona kama ushaanza kumjaa mdogo wng Harmonize anaonekana kujitenga sana crew ya wasafi anajiona ashakuwa mkubwa. Nikuhakikishie Harmonize hawa wanaokujaza bichwa hawakutakii mema na siku ukijitoa wasafi baada ya miezi kadhaa hutowasikia tena watahamia kwa msanii mwingne na kuanza kukuponda.

Diamond ni msanii pendwa ana maadui wengi na mashabiki wengi sana so hao maadui ndo hutafuta kila mbinu ya kumwngusha ndo maana kila leo wanakuja na mbinu tofauti tofauti ili tu kum-frustrate bwana mdogo ila yeye ashaamua kukaza ndo maana mpk leo yupo hapo. Acha kusikiliza huu upepo maana ni wa mda tu, kumbuka Domo kakutoa wapi kakupiganiaje mpk leo upo hapo. Ukitaka kujua hilo kaangalie upya interview yako ulofanya mara ya kwanza na Millard Ayo itakupa funzo upya. Usipelekwe na huu upepo wa mda ambao baadaye utakugeuka.

By Kifimbocheza_