MREMBO wa miaka yote, Wema Sepetu amesema hata kama amepungua mwili kiasi gani lakini anajivunia kwamba bado kalio lake lipo vilevile.  Wema aliyasema hayo hivi karibuni alipokutana na mwanahabari wetu na kupiga naye stori ambapo alisema, hata kama watu wanalalamikia kukonda kwake yeye haimsumbui hata kidogo sababu kalio liko vilevile.

“Hahahaha! Najua wengi wananisema kuhusu kupungua lakini mimi hata sijali maana kalio langu lipo vilevile, halijapungua hata kidogo, najivunia kuwa hivi nilivyo sasa na siwezi kuwaridhisha watu wote niwe kama wanavyotaka wao,” alisema Wema ambaye miezi kadhaa iliyopita alijipunguza mwili wake bila kuweka wazi hasa siri ya alichofanya

GPL