HIVI unajua miaka inaenda na watu wanabadilika tabia? Leo hii unaweza kuamini staa wa filamu Bongo Muvi, Wema Sepetu anaifurahia mimba ya mchumba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,Tanasha Donna tofauti na watu wanavyodhani labda anaumia au hafurahishwi na mimba ya mrembo huyo.Akipiga stori mbili tatu na Za Motomoto ya Risasi, Wema alisema kuwa kubeba ujauzito ni jambo la kheri sana na ni Baraka kwa kila mwanamke hivyo alivyosikia Tanasha kapata ujauzito alifurahi na pia anaamini baba wa ujauzito huo anapenda watoto pia.

“Mimi kwa kweli namfurahia Tanasha sana na ninamuombea Kwa Mungu alete heri kwake, kwa sababu ukiona mwanamke yupo katika hatua hiyo mpongeze na umuombee kwa Mungu amalize kazi hiyo salama.Pia ninachofurahia baba wa mtoto huyo anapenda sana watoto na hilo ni jambo heri,” alisema Wema ambaye aliongeza kuwa japokuwa hana tatizo na Diamond lakini kama akija na kumuomba wazae mtoto kamwe hawezi kukubali kwani penzi lao lilishakufa muda mrefu.