KAMA ulikuwa na mawazo kwamba huenda mwigizaji mahiri Bongo, Wellu Sengo na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wanaweza kuendeleza mapenzi, sahau! Mrembo huyo amezidi kusisitiza kuwa biashara imeisha.


Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Welu ambaye wiki chache zilizopita aliweka wazi kwenye mtandao wake wa Instagram kuwa yupo ‘singo’ alisema kuwa siyo kitu kibaya kuandika vile kwa sababu kila mtu ana mtazamo wake.


“Kiswahili mara nyingi huwa kigumu, lakini ukweli ni kwamba Nyerere ni baba mtoto wangu na hakuna kingine zaidi ya hicho, watu waelewe na ninamshukuru Mungu hakuna kinachonisumbua kwa sasa,” alisema Welu.

STORI: IMELDA MTEMA,DAR