Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu ametoa tahadhari ya Ugonjwa wa Ebola kwa Wananchi katika mikoa yote ya Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, imetoa elimu kwa watanzania juu ya namna ya kuepuka ugonjwa huo ambao ni hatari.

Waziri Ummy amewataka wananchi kuchukua hatua stahiki za kujikinga na kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini.

Ebola imekuwa tishio kwa nchi kadhaa zinazopakana na Tanzania ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Wizara ya Afya Tanzania
@wizara_afyatz
 Wizara inapenda kutoa Tahadhari ya Ugonjwa wa Ebola kwa Wananchi katika Mikoa yote ya Tanzania na pia kuwataka kuchukua hatua stahiki za kujikinga, na kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini mwetu@Waziri Ummy Mwalimu#TaarifaKwaUmma@umwalimu@DocFaustine