\
Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akimwelezea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu hali ya ununuzi wa pamba kutoka kwa wakulima unavyoendelea katika kiwanda cha Kuchambua pamba cha Fresho kilichopo katika eneo la Ibadakuli Mjini Shinyanga alipotembelea Kampuni ya Fresho Investment Company Limited leo Agosti 9,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia pamba katika kiwanda cha Fresho. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko,akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akimuonesha na kumwelezea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa pamba iliyoletwa na wakulima katika kiwanda cha Fresho.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia pamba iliyoletwa na wakulima katika kiwanda cha Fresho.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia pamba iliyoletwa na wakulima katika kiwanda cha Fresho.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza wakati akiangalia pamba iliyoletwa na wananchi katika kiwanda cha Fresho.
Wakulima wakiwa na pamba yao katika kiwanda cha Fresho.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akiwasalimia wakulima wa pamba walioleta pamba yao katika kiwanda cha Fresho.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Wanunuzi wa pamba mkoani Shinyanga,Gasper Kileo wa kiwanda cha GAKI (aliyevaa shati la kijani kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho,Fredy Shoo
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho,Fredy Shoo akimweleza jambo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akielekea katika kiwanda cha kuchambulia pamba cha Fresho.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiingia Ginnery C.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia pamba iliyochambuliwa katika Ginnery C,ambapo kuna Ginnery A,B,C na nyingine ipo wilayani Kahama,zote zikimilikiwa na Kampuni ya Fresho.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiongozwa kiwandani.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungungumza jambo katika kiwanda cha Fresho.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akitoka Ginnery C.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wakulima wa pamba na wananchi katika kiwanda cha Fresho.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Fresho wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akisoma taarifa fupi kuhusu kiwanda cha Fresho na hali ya ununuzi wa pamba.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akisoma taarifa fupi kuhusu kiwanda cha Fresho na hali ya ununuzi wa pamba.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akiteta jambo na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza katika kiwanda cha Fresho.
Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mhe. Gulam Hafeez Mukadam,kulia ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM).
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Solwa,Mhe. Ahmed Salum na Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Mhe. Nyabaganga Talaba.
Picha ya pamoja viongozi mbalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa.
Magari yaliyoleta pamba yakiwa nje ya kiwanda cha Fresho.
Sehemu ya pamba iliyoletwa na wakulima kuuzwa katika kiwanda cha Fresho.
Sehemu ya pamba iliyoletwa na wakulima kuuzwa katika kiwanda cha Fresho.
Sehemu ya pamba iliyoletwa na wakulima kuuzwa katika kiwanda cha Fresho.
Sehemu ya pamba iliyoletwa na wakulima kuuzwa katika kiwanda cha Fresho.
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha Kuchambua pamba cha Fresho kilichopo katika eneo la Ibadakuli Mjini Shinyanga na kujionea hali halisi ya ununuzi wa pamba kutoka kwa wakulima unaofanywa na Kampuni ya Fresho Investment Company Limited.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha Fresho kinachomilikiwa na Kampuni ya Fresho Investment Company Limited leo Ijumaa Agosti 9,2019 wakati akiwa kwenye ziara yake ya siku moja mkoani Shinyanga.
Akizungumza kiwandani hapo,Waziri Mkuu aliwahakikishia wakulima wa pamba kuwa pamba yao itanunuliwa kwani lengo la serikali ni kuondoa pamba mikononi mwa wakulima.
"Nipo kwenye ziara kwenye mikoa inayolima pamba lengo la kufuatilia mwenendo wa masoko ya pamba. Nikiwa hapa Shinyanga nimeshuhudia wingi wa pamba inayoletwa na wananchi kwenye masoko,kwetu sisi kama serikali ni jambo kubwa sana kiuchumi kwani pamba kwa Tanzania ni uchumi mkubwa,pamba imetupa heshima",alisema Majaliwa.
"Natumia fursa hii kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo pamoja mama Fredy na watoto wa Fredy na watumishi wote wa Fresho,mnafanya kazi kubwa sana ya kuunga mkono jitihada za serikali kwa kununua pamba,nikiwa nazunguka kwenye mafurushi ya pamba kule nje,ameniambia mule ndani ni zaidi imeshanunuliwa na wanaendelea kuilipia na bado magari yanaingia kuleta pamba",
"Kilichonifurahisha zaidi ni ile kauli yake kwamba 'Nitalipa pamba yote' yupo tayari kununua pamba yote. Kampuni ya Fresho mnafanya jambo jema kununua pamba,sisi kama serikali tunakushukuru sana na tutakulinda,hatutakuangusha. Hapa kuna mkuu wa mkoa,ukipata tatizo usisite kumuona",alisema.
Hata hivyo Majaliwa aliwapongeza wakulima kwa kuzingatia usafi kwenye pamba kwa kuachana na tabia ya kuweka maji,mchanga,mafuta na takataka mbalimbali zinazosababisha pamba ichafuke na kuchangia sasa pamba ya Tanzania inapendwa duniani kote.
Aidha aliwataka wakulima wa pamba kuiga wakulima wa korosho kwa kufungua akaunti benki badala ya kutembea na mafurushi ya fedha kwa siyo salama.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumhamasisha Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho,kuanzisha kiwanda cha kusokota nyuzi za pamba na kiwanda kiwanda cha kutengeneza nguo.
Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu,Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Limited, Fredy Shoo alisema mbali na kumiliki kiwanda cha kuchambulia pamba pia wana kiwanda cha vifungashio na kiwanda cha kuchakata mafuta ya pamba.
Alisema mwaka huu,kampuni yao ipo katika soko la ununuzi wa pamba kwa uwezeshaji wa benki ya NBC na CRDB ambapo mpaka sasa wamenunua pamba kilo milioni 26.5 kati ya hizo kilo milioni 24 zimeshapokelewa kiwandani na wanaendelea kununua pamba kutoka kwa wakulima.
Alieleza kuwa pesa kutoka benki zimepungua hali inayochangia kupunguza kasi ya ununuzi wa pamba huku akisisitiza kuwa kampuni ya Fresho inategemea kununua pamba nyingi kadri inatakavyowezekana endapo watapata fedha zaidi.
"Kampuni yetu imebeba dhamana kubwa ya kununua pamba licha ya changamoto kubwa ya soko,hii yote tunafanya ili kumpunguzia adha mkulima lakini pia kuunga mkono jitihada za serikali kutaka pamba ya mkulima inunuliwe",alisema Shoo.
"Pamoja na changamoto ya soko la dunia kuwa chini, Tumeendelea kununua pamba kwa bei ya shilingi 1,200/= kama serikali ilivyoagiza na baadhi ya wakulima wamekuwa wakileta pamba yao hapa kiwandani nyingine ni ile inayonunuliwa na wamachinga kwa bei ya chini tofauti na iliyoelekezwa na serikali hali inayowapa hasara wakulima",alisema Shoo.