Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amemuomba Rais Magufuli uwekwe utaratibu kwa ajili ya kulifanyia ukarabati wa Jengo la pili la Abiria ili liwe na uwezo wa kubeba abiria wengi zaidi.


Waziri Kamwelwe ameyabainisha hayo leo Agosti 1 wakati wa uzinduzi wa Jengo la tatu la abiria (Terminal III) katika uwanja wa ndege wa julius Nyerere.

'Ombi langu kwako Mh Rais,  jengo lile Terminali II  linahitaji mambo mawili, moja  kuikarabati ipendeze kama ambavyo wamependeza wananchi waliokusanyika hapa kama alivyosema Makonda ''Wameoga'',lifanyiwe marekebisho ili nalenyewe ling'are  kama jengo la tatu lilivyo, pili katika kukarabati huko liongezewa capacity ikiwezekana mara mbili badala ya kubeba abiria milioni 1.5 libebe abiria milioni 3'' amesema Waziri Kamwelwe.

Jengo la tatu la abiria (TERMINAL III) katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 560 na litakuwa na uwezo wa kubeba abiria milioni 6 kwa mwaka