Waziri Jaffo Atoa Onyo Kali Kwa Wanaoleta Chokochoka kipindi Cha Uchaguzi
“Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, na hivi karibuni tunakwenda kupiga kura kuchagua viongozi wa serikali za mitaa.

 Kuna watu wanatumia kipindi hiki kuleta chokochoko, niwaambie…tumejipanga kulinda amani kabla na baada ya uchaguzi,”

Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo akihutubia Baraza la Eid linalofanyika katika viwanja vya Masjid Kibaden Chanika Zogowali Ilala jijini Dar es salaam.