PASCAL Wawa, beki wa Simba maarufu kwa jina la Sultan amesema mashabiki wasiwe na presha kuelekea mchezo wa marudiano wa kimataifa dhidi ya UD do Songo unaochezwa Agosti 25.Habari njema nyingine kwa mashabiki wa Simba ni kwamba hata Ibrahim Ajibu na Aishi Manula nao wameshuka uwanjani tayari kuendelea kupiga mzigo baada ya kupata mushkeri kidogo wa majeraha.Simba ambayo ndiyo klabu yenye kikosi ghali zaidi msimu huu nchini Tanzania, inacheza Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mchezo wa kwanza wa awali wakiwa Msumbiji iliambulia suluhu.Akizungumza na Spoti Xtra ambalo ndiyo gazeti bora kwa sasa la michezo linalotoka kila Alhamisi na Jumapili, Wawa ambaye ni mchezaji wa zamani wa Azam, alisema kuwa mchezo wa marudio utakuwa mgumu ila watapambana kupata matokeo chanya kwa kuwa watakuwa nyumbani.“Mechi za kimataifa zina ushindani wake na kila timu inahitaji kusonga mbele kwa sasa tunajipanga kurudiana nao nyumbani, imani yetu tutapata matokeo mazuri.“Kwa sasa hakuna haja ya kuwa na presha kubwa kwani makosa ambayo tuliyafanya mchezo wa kwanza yamefanyiwa kazi na tunawaomba mashabiki watupe sapoti,” alisema mchezaji huyo raia wa Ivory Coast na swahiba wa Didier Drogba.Simba wanahitaji ushindi wa aina yoyote kwenye mchezo huo wa marudiano ili kufuzu raundi ya kwanza ya michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu ambayo msimu huu ilianza wikiendi iliyopita.