Madereva wawili na Wafanyabiashara wanne wa Madini ya Dhahahu wamenusurukika kwenda jela miaka 20, baada ya kulipa faini ya zaidi ya Shilingi Milioni 341, baada ya kukiri kosa la kusafirisha la madini ya yenye thmanai ya zaidi ya Shilingi bilioni 2.

Katika fedha hiyo wa Mil. 341, kiasi cha Sh.Mil 125 ni faini na Sh.Mil 216.5 ni fidia wanayotakiwa kulipa kutokana na kuisababishia Serikali hasara.

Hukumu hiyo imetolewa na  Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam, Janeth Mtega baada ya washtakiwa hao kwa ujumla wao kukiri makosa yao na Mahakama ikawatia hatiani na kuwahukumu.

Akiwasomea hukumu hiyo Hakimu Mtega amesema washtakiwa kwa pamoja walishiriki genge la uhalifu, kusafirisha madini nje ya nchi, kuuza madini kinyume na sheria, kushindwa kulipa mrabaha na kuisababishia hasara Serikali.