Wakazi na Nikki Wa Pili wametoa neno kuhusu utata uliotokea kwenye mtandao ya kijamii wa Instagram kuhusu 'Producer' P Funk Majani na Profesa Jay.


Wasanii hao wametoa maoni yao kupitia EATV & EA Radio Digital baada ya posti hiyo kusambaa katika mitandao wa kijamii wa Instagram ikimuonyesha P-Funk Majani akimtupia maneno Prof.Jay kwenye post aliyoweka.

Kwa upande wa rapa Wakazi amesema, “mimi naona maoni ya Prof.Jay hayana tatizo lolote kwa sababu alikuwa anachanganua kuhusu kauli iliyotolewa na COSOTA kwamba haikuwa sahihi na wala hakulipwa pesa bali aliwataka warekebishe kauli yao”.

Wakazi ameendelea kusema kuwa maneno ya P-Funk Majani yalitokana na kutoelewa alichokiandika Prof. Jay na alifikiri posti aliyoweka ilikuwa anamuongelea na kuingilia upande wake.

Aidha kwa upande Nikki wa Pili amesema kilichotokea ni kutoelewana na anafikiri Prof.Jay hakumshambulia P-Funk, ila alitoa maelezo kuwa mirabaha imelipwa na haikupitia kwake na kauli waliyoitoa COSOTA haikuwa sahihi.

Pia Nikki wa Pili ameendelea kusema kuwa kuhusu posti ya P-Funk Majani ni kwamba ilitafsiri vibaya kwa kudhani kitendo cha kupewa mirabaha Prof.Jay atakuwa hajakipenda.