Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kuanza vikao vya kamati za kudumu siku ya Jumatatu tarehe 19 Agosti hadi tarehe 02 Septemba 2019, Jijini Dodoma, kabla ya kuanza kwa mkutano wa kumi na sita wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 3 Septemba 2019.

Taarifa iliyotolewa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa cha Bunge leo Ijumaa 16 septemba 2019 imesema pamoja na mambo mengine kamati tisa za sekta na kamati ya bajeti zitachambua taarifa za taasisi na wizara za Serikali kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali.

Mbali na kupokea taarifa mbalimbali za wizara/taasisi, kamati hizo zitachambua taarifa ya CAG.

Shughuli nyingine zitakazofanywa na kamati hizo ni pamoja na uchambuzi wa sheria ndogo, pamoja na uchambuzi wa taarifa za uwekezaji wa mitaji ya umma.