Idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali ya moto wa lori la mafuta mkoani Morogoro imefikia 102 baada ya majeruhi mmoja aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kufariki dunia.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha amemtaja aliyefariki ni Grayson Ndabiti (19) hivyo idadi ya majeruhi waliobaki hospitalini hapo ni 13.

Amesema kati ya majeruhi hao saba wako chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku wengine sita wakiwa katika wodi ya Sewahaji.