Bado ni vichwa vya habari kuhusu simanzi na huzuni zinazoendelea kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva baada ya kufariki kwa msanii Mbalamwezi anaetokea katika kundi la The Mafik.

Sasa hapa tumempata msanii kutoka kundi la Makomando ‘Muki’ ambae kupitia Ayo TV amefunguka kuhusu kifo msanii mwenzake ‘Mbalamwezi’ na kuwaasa vijana kutulia kuacha tamaa kuwa na uvumilivu.