PENZI jipya mjini! Staa wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya na Mbongo- Fleva kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Abdul Iddi ‘Lava Lava’ kwa sasa uhusiano wao siyo siri tena, Gazeti la Ijumaa Wikienda linakupa mkanda kamili.  Siri ya wawili hao ilifichuka hivi karibuni kwenye baby shower ya mpenzi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna iliyofanyika kwenye Hoteli ya Best Western Coral Beach, Masaki jijini Dar.

Uwoya na Lava Lava walitinga kwenye shughuli hiyo wakisindikizana na kubembelezana kimahaba huku baadhi ya watu wanaoujua ukaribu wakisema; “Si tulisema ni wapenzi mkabisha?” Tukio hilo ndilo lililothibitisha uhusiano wao ambao umekuwa wa kujifichaficha. Mambo yalikuwa hivi; Uwoya ndiye aliyeanza kuingia ukumbini ambapo alikwenda kuketi na kwenye siti ya ubavu wake wa kulia aliweka kipochi chake ili asikae mtu mwingine.

Baada ya muda mfupi, Lava Lava naye aliingia eneo la tukio na kuonekana akiangaza pakukaa kisha akanyoosha moja kwa moja hadi kwa Uwoya ambapo alipofika alilakiwa kimahaba. Picha haikuishia hapo kwani wawili hao ni kama walikuwa wamechoka kuficha mambo yao kwani ilifikia wakati walipokuwa wakitaka kuinuka na kwenda sehemu walikuwa wakitembea kimahaba huku Lava Lava akilishikilia kimahaba gauni la Uwoya.

Wawili hao, kila mmoja alionekana kumnyenyekea mwenzake wakati wakivinjari kwenye bustani za hoteli hiyo. “Walificha weee…hadi wamechoka, sasa siyo siri tena, wameamua kuweka mambo hadharani,” alisikika mmoja wa wageni waalikwa wa shughuli hiyo akimuambia mwenzake